ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 8, 2017

Rais Museveni abadilisha tarehe yake wa kuzaliwa

Kwa muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni.

Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena.
Lakini nadhari nyingine imeibuka  ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na hivyo sasa ana miaka 70.
Kwa minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea tena katika awamu ya sita.

Museveni alibadilisha katiba ya Uganda mwaka 2006 ili kuweza kugombea awamu ya tatu.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini humo, Rais amewahi kusema kwamba hafahamu tarehe yake ya kuzaliwa.

“Wazazi wangu hawakwenda shule na hivyo hawakujua tarehe,” alinukuliwa Rais Museveni mwaka 1997 alipokuwa akitoa taarifa zake katika mahojiano maalum.

Mkanganyiko huu umekuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu Rais Museveni aliposema kuwa katika kipindi cha miaka 31 alichokuwa madarakani hajawahi kuugua.

“Umewahi kusikia Museveni ameumwa na miguu yake kuning’inizwa hospitalini kwa miaka 31 iliyopita? Hii ni kwa sababu nafuata hatua za msingi za afya ambazo zimenisaidia kuepukana na magonjwa. Magonjwa haya yanaweza kuzuilika,” alisema Museveni akitamba kwamba afya yake ni imara.

No comments: