Sunday, August 27, 2017

SHULE YAKOSA OFISI YA WALIMU KWA MIAKA 14.

Shule ya msingi Mlimwa B iliyoko manispaa ya Dodoma haina ofisi za walimu huku zaidi ya walimu 30 wakilazimika kugeuza madarasa kuwa sehemu ya kufanyia kazi zao hali inayowaondolea umakini kwa kuwa wanachanganyika na wanafunzi muda wote.

Shule hiyo iliyoanzishwa tangu mwaka 2003 ina wanafunzi 750 haina ofisi za walimu na ile ya mwalimu mkuu ambapo walimu wanasema wamegawana vyumba vya madarasa kwa ajili ya kufanyia kazi zao ambapo kila chumba wanakaa walimu watano.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Stan Mwalongo anaiomba serikali na wadau wa maendeleo kuijengea shule hiyo jengo la utawala ili walimu wapate ofisi zao huku akisema kukosekana kwa ofisi kunaathiri maendeleo ya taaluma shuleni hapo.

Kufuatia adha hiyo mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme ameanzisha harambee maalum ya kuchangia fedha za ujenzi wa ofisi ya walimu sambamba na kuzindua vyoo vya wanafunzi shuleni hapo vilivyojengwa kwa msaada wa wakala wa bima wa Jubilee kama sehemu ya kurejesha faida wanayoipata kwa jamii .

No comments: