Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu amesema kamati ya ulinzi na usalama imekamilisha utaratibu wa kuwasaka wanafunzi wenye mimba ili kuchukua hatua.
Aliitoa kauli hiyo juzi akiwa Kata ya Ntobo katika Halmashauri ya Msalala wakati wa makabidhiano ya mradi wa maendeleo ya jamii wa ADP Busangi uliokuwa ukitekelezwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kuishirikisha wananchi.
Alisema pamoja na mafanikio ya mradi huo, Nkurlu ambye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, alisema kwa sasa tayari utaratibu wote kupitia kamati zote za ulinzi na usalama za mji, Msalala na Ushetu zimekaa na kukubaliana kuwasaka shule hadi shule wasichana watakao kuwa na mimba.
“Baada ya kukubaliana kitakaochofuata ni kuwakamata na wale watakaobainika hatua kali zitachukuliwa, Serikali haiwezi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya watoto kwenda shule lakini yanafanyika mambo kinyume,” alisema.
Kaimu mkurugenzi wa shirika hilo, Johnson Robinson alisema utekelezaji wa mradi huo umeiinua sekta ya elimu.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment