ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 7, 2017

JOCKTAN MAKEKE KUSHIRIKI MAONESHO YA UTAMADANI NCHINI NIGERIA

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan Makeke leo asubuhi.
Msanii wa mitindo inayohusu utamaduni wa Mwafrika Jocktan Makeke / MAKEKE INTERNATIONAL  leo hii anatarajia kwenda Abuja Nigeria kwa ajili ya maonesho makubwa ya utamaduni ya FACE OF CULTURE NIGERIA, ambapo ataonesha mavazi yenye ubunifu wa hali ya juu ambayo yanakwenda kwa jina la #OTOSIM2017
Tamasha hilo litafanyika siku ya tarehe 09/09/2017 katika ukumbi wa Sheraton Hotel ya mjini Abuja.
Aidha maonesho hayo yataambatana na utoaji wa tuzo kwa watu mbalimbali ambao wamefanya vizuri kwenye mambo ya utamaduni.

No comments: