
Mtoto wa wiki nne ameokotwa pembezoni mwa barabara ya mwendo kasi I 40 jimbo la Oklahoma akiwa maeachwa na mama yake kwenye ndani ya kiti chakumbembea mtoto ndani ya gari.
Mtoto huyo alikutwa maechwa na pesa taslimu $6,000, diski mweko (flash drive), cheti chake cha kuzaliwa na na namba yake ya usalama SSN.
Mtoto hyuyo aligunduliwa na watumia barabara hiyo baada ya kuona kiti cha gari cha mtoto kikiwa futi 10 pembezoni mwa barabara hiyo huku mtoto huyo akiwa kwenye usingizi mzito bila kufahamu kilichotokea.
Polisi wa Oklahoma ameeleza mama wa mtoto huyu amepatikana lakini hawakueleza ni hatua gani atakazochukuliwa na bado haijajulikana sababu za mama huyo kumtelekeza mwanae pembezoni ya barabara ya mwendo kasi.
No comments:
Post a Comment