ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 22, 2017

SPIKA JOB NDUGAI AHUDHURIA MAZISHI YA FAMILIA YA ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiwasili katika Msiba wa familia ya  Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa Mjini Mhe. Gregory George Teu uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, ambapo mazishi yatafanyika mapema leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimfariji Mbunge Mstaafu wa Mpwapwa Mjini Mhe. Gregory George Teu (kushoto) kwa Msiba wa familia yake uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, kabla ya kuanza kwa mazishi yatafanyika leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.

 Wananchi Mbali mbali waliohudhuria  katika Msiba wa familia ya  aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu uliotokea tarehe 18 Septemba, 2017 nchini Uganda, katika mazishi yaliyofanyika  leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, katika msiba uliofanyika leo nyumbani kwake Mpwapwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika misa ya kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, uliofanyika leo katika kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa)iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiweka Shada ya maua katika mazishi ya familia ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, yaliyofanyika leo katka makaburi ya kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa) iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma.

No comments: