Advertisements

Saturday, October 21, 2017

Madakitari kutoka San Francisco - California Watembelea kituo cha Mafunzo Muhimbili - MUHAS

Jopo la madakitari kutokea University of California San Francisco (UCSF) kitivo cha magonjwa ya  saratani walipata fursa ya kusafirini na kuelekea Tanzania mwanzoni wa mwezi Septemba 2017. Wataalamu hao walipata fursa kufika kitivo cha Muhimbili Tanzania (MUHAS) na kutoa mafunzo na utaalamu katika matibabu ya magonjwa saratani.  Mwenye suti ya kijivu na shati la bluu ni mdau Walter Minja aishie California akifurahia na kuwashukuru madakitari hao kwa hatua kubwa waliochukua kwenda nchini Tanzania na kutoa huduma hiyo muhimu.
 Wataalamu wa taasisi ya mafunzo Muhimbili - MUHAS wakipata picha ya pamoja na wadau kutoka Marekani baada ya kuhitibu mafunzo. Katika mwenye mawani ni Vice Chancellor wa MUHAS Prof. Kaaya
 Vice Chancellor wa MUHAS Prof. Kaaya akitoa zawadi ya kushukuru wa jopo la wataalamu waliokwenda Tanzania kutoa huduma hiyo muhimu ya utabibu wa magonjwa ya saratani.
 Pichani Prof. Kaaya akimkabidhi  mmoja wa waatalamu kutoka Marekani ambaye ni Associate Director wa Global Cancer Program Deirdre Olynick zawadi ya kushukuru kuongoza jopo zima wa madakitari.
 Mdau Walter Minja akifuatilia kwa makini maada iliyokuwa inatolewa na Director wa Global Cancer Program Dr. Katherine Van Loon hayuko pichani.