Leo Jumamosi Oktoba 7,2017 kumefanyika mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mbali na kufanyika kwa mahafali hayo ya darasa la saba pia kumefanyika mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) sambamba na uzinduzi wa Bendera na Wimbo wa shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wazazi na wadau mbalimbali wa elimu alikuwa Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi”.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ilianzishwa Julai mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi 12 na kwamba mwaka huu ndiyo mara yao ya kwanza kufanya mahafali wakiwa na wahitimu 35.
“Tulianza na wanafunzi 12 katika chumba cha gereji huko Mwasele,leo shule ina jumla ya wanafunzi 622,waliohitimu mwaka huu ambao tunawafanyia mahafali ni 35,hii ni hatua nzuri tunamshukuru Mungu na wazazi ambao wamekuwa bega kwa bega nasi kuhakikisha shule hii inafanikiwa”,alieleza Dominic.
Naye Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita aliipongeza bodi ya shule, walimu,wafanyakazi wa na wazazi kwa ushirikiano walionao katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inatoa elimu bora kwa wanafunzi.
Katika hatua nyingine Mwita alisema ili kuinua kiwango cha elimu,wameanzisha ujenzi wa shule ya sekondari na wanafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanapata usajili ili shule ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwaka 2018.
Aidha aliwaomba wazazi na wadau wa elimu kuendelea kutoa ushirikiano katika kukamilisha ujenzi unaoendelea wa jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” .
Akitoa hotuba yake,mgeni rasmi Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products aliipongeza shule hiyo kuendelea kutoa elimu bora na kuwa na mazingira bora ya kujifunzia hali inayosababisha watoto wakue vyema kiakili,kimwili na kimaadili.
“Msingi mzuri wa elimu kwa mtoto ni kuanzia shule ya msingi hivyo nawasihi wazazi kupeleka shule,serikali yetu inapigania viwanda,viwanda hivi vinahitaji rasilimali watu,lazima tuwapatie elimu hawa watoto wetu ili maarifa wanayopata wayatumie katika viwanda hivi”,aliongeza.
Hapa ni katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba na mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) yaliyofanyika leo Jumamosi Oktoba 7, 2017.
Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Wazazi na walezi wakiwa katika mahafali hayo
Mgeni rasmi bwana Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi” akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Muonekano wa eneo la mahafali
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Little Treasures Tilulindwa Sulus akizungumza katika mahafali hayo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Paul Kiondo akizungumza wakati wa mahafali hayo
Awali wanafunzi wa shule ya Little Treasures wakiandamana kutoka Mwasele ambako ndiko shule hiyo ilianzia kabla ya kuhamia Bugayambelele kata ya Kizumbi.
Wahitimu wa darasa la awali "Pre Unit" wakiingia ukumbini
Wahitimu wa darasa la awali wakiingia ukumbini
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia wawili wawili ukumbini kwa madaha
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini kwa kucheza
Wanafunzi wakiimba wimbo wa taifa
Mgeni rasmi akivalishwa skafu
Bendera rasmi ya shule ya Little Treasures Nursery & Primary School ikipandishwa kwa mara ya kwanza ambapo pia wakati wa mahafali hayo wimbo maalum wa shule hiyo ulizinduliwa.
Wahitimu wa darasa na saba wakiwa wamekaa na wazazi wao
Wahitimu wa darasa la saba
Wahitimu wa darasa la awali wakiwa eneo la tukio
Wahitimu wa darasa la awali wakiwa katika eneo la tukio
Wahitimu wa darasa la awali wakisalimia kwa kunyoosha mikono
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo
Mwalimu Joyce Pius akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi wa shule hiyo
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wakifungua shampeni...
Meza kuu wakipata vinywaji baada ya shampeni kufunguliwa
Wanafunzi wa darasa la awali wakikata keki maalum kwa ajili yao
Wahitimu wa darasa la saba wakikata keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao
Wahitimu wa darasa la saba wakiendelea kukata keki
Mhitimu wa darasa la saba akimlisha keki mgeni rasmi bwana Saleh Shaban Mohammed.
No comments:
Post a Comment