ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 31, 2017

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA UZINDUZI WA MRADI WA KUJENGA UWEZO KWA TAASISI KATIKA UDHIBITI WA KEMIKALI NA TAKA SUMU.

 Mgeni Rasmi katika warsha ya uzinduzi wa Mradi wa kujenga uwezo kwa Tasisi katika udhibiti wa kemikali na taka sumu , Bwana Richard Muyungi ambaye ni Mkurugenzi idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akiongeakatika uzinduzi wa warsha hiyo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga akiongea wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira.
 Sehemu ya Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Mwakilishi wa UNEP  Bibi Nalimi Sharma akiongea katika warsha hiyo, pembeni yake Mkurugenzi wa Mazingira Ofsis Ya Makamu wa Raisambaye  ni Mgeni Rasmi Bwana Richard Muyungi
 Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali.

Nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu. Taka sumu nyingi zimekua tishio kwa Wananchi hasa Wanawake na Watoto. Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi  ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,  Bwana Richard Muyungi alipokua akifungua warsha ya uzinduzi wa mradi wa kujenga uelewa kwa Taasisi za Serikali katika udhibiti na usimamizi wa kemikali na taka sumu jijini Dar Es Salaam.
Pia ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kwa msaada wa kifedha katika kuanzishwa kwa mradi huo, ameongeza pia  Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo wakaitumie vema elimu watakayoipata katika sehemu zao za kazi ili kuongeza weledi na maarifa.
Akiongea katika warsha hiyo Mwakilishi kutoka UNEP Bi.Nalimi Sharma amesema amefurahi sana kuhushuria uzinduzi wa warsha ya mradi huo na kuona jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika suala zima la usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu. Ameongeza kuwa UNEP itaendelea kutoa msaada wa kifedha kwa kwa Ofisi ili kuendelea kuimarisha shughuli za usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu. 

No comments: