Nyuku vikiwa vipo tayari kwenye picnic ya familia na nyama choma iliyoandaliwa na Shield Our Watoto siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio. SOW ni oganaizesheni iliyoanzishwa na Bhoke Kirigiti akishirikiana na mumewe PeterKirigiti inayotetea watoto kutokana na unyanyasaji hasa watoto wa kike inapowapigania hasa unyanyasaji wa kingono chini ya umri mdogo. Oganaizesheni hii hushirikiana na wazazi wa watoto na watu mbalimbali wakiwemo watoa elimu ya unyanyaswaji wa watoto wakishirikiana na mashirika mbalimbali yasiyokua ya Kiserikali. Shield Our Watoto hutoa elimu ya bure kwa wazazi na watoto kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa watoto wenye umri ndogo ambao kati ya watoto 3 kati ya 10 wamekua wakiathirika kisaikolojia kutokana unyanyasaji huo
Peter Kirigiti pamoja na mkewe Bhoke Kirigiti wakielezea Shield Our Watoto (SOW) kwa wadu waliohudhuria family picnic na nyama choma siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio.
Wadau mbalimbali waliojumuika kwenye nyama choma hiyo wakiwasikiliza PeterKirigiti na mkeweBhoke Kirigiti.
Clara Ijames mwandishi wa kitabu cha There's Beauty Inside akielezea unyanyasaji wa watoto hasa kwa mtoto wa kike unawezaje kuathiri saikolojia katika maisha yake.
Rebecca Walters (mwenye miwani) akiwalekeza watoto jinsi ya michezo yao itakavyochezwa.
Rebecca Walters na Keri Willard (aliyeengemea ukuta) ambao ni wanafunzi wanaosomea MA Counseling Ministries-Pastoral and Professional Counseling katika chuo cha Methodist Theological cha Ohio (MTSO) wakijitolea kucheza na watoto ikiwemo kuwafundisha michezo mbalimbali ya watoto.
Rebecca Walters na Keri Willard (kushoto) wakiwaonyesha watoto michezo yao.
Watoto wakikimbia huku wakiwa wamefunga miguu yao kwa pamoja na mkanda.
Watoto wakifurahia kucheza na mipira aina ya maputo
Watoto wakicheza kwenye michezo yao.
No comments:
Post a Comment