Familia inawashukuru mno kwa muda na upendo wenu, hatuna cha kuwalipa kitakacholingana na wena, upendo, mshikamano na kujitolea kwenu na bila kujali muda wenu Mimi Kenyatta na kwa niaba ya familia yangu tunasema asante na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awaongezee mara mbili ya hicho mlichopunguza kwa ajili ya familia hii,
Asanteni wote na tunashukuru mno
Prof Boas (kushoto) akiwa pamoja na mfiwa Kenyatta Mayanga mapema kwenye kisomo cha mpendwa dada yake Mgeni Mayanga kilichofanyika siku ya Jumapili Oktoba 8, 2017
Magie na Sara (kulia) wakijumuika nyumbani kwa Kenyatta Mayanga Takoma Park siku ya JumapiliOktoba 8, 2017 kwnye kisomo cha mpendwa dada yake Mgeni Mayanga aliyefariki Tanzania mapema wiki iliyopita
Kisomo cha kumwombea mpendwa dada yake Kenyatta marehemu Mgeni Mayanga siku ya Jumapili Oktoba 8, 2017 Takoma Park, Maryland.
WanaDMV na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye kisomo cha mpendwa dada yake Kenyatta Mayanga marehemu Mgeni Mayanga aliyefaki Tanzania wiki iliyopita, kisomo kilifanyika siku ya Jumapili Octoba 8, 2017 Takoma Park, Maryland.
No comments:
Post a Comment