Oktoba 13 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa. Maadhimisho haya ni utekelezaji wa Azimio Na. 64/200 lililopitishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa tarehe 21 Desemba, 2009. Siku hii inalenga kukuza utamaduni wa usimamizi wa maafa kimataifa, ikiwa ni pamoja
na kuzuia, kupunguza madhara,
kujiandaa, kukabili na kurejesha hali katika ubora zaidi pale maafa yanapotokea.
]
Ndugu Wananchi,
Katika kuadhimisha siku hii, Sekretarieti ya Upunguzaji wa Madhara ya
Maafa ya Umoja wa Mataifa (United
Nation Strategy for Disaster
Reduction - UNISDR) hutoa Kaulimbiu
ya mwaka husika. Kaulimbiu
ya mwaka huu inasema:
“MAKAZI SALAMA: Punguza
Makazi katika Maeneo Hatarishi,
Punguza Kuhama kutokana
na Maafa”
(HOME SAFE HOME: Reducing Exposure, Reducing Displacement).
Siku hii ni fursa ya kutambua
maendeleo makubwa yanayofanywa
katika kuleta matokeo
ya kupunguza hatari na madhara
ya maafa katika maisha, mifumo ya maisha na afya, kiuchumi, kijamii,
kiutamaduni na rasilimali za mazingira.
Matokeo hayo ni lengo la Mkakati wa Sendai wa Kupunguza Madhara
ya Maafa wa 2015 – 2030.
1
Mwaka jana Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa alifanya uzinduzi wa "Kampeni ya Malengo Saba ya
Sendai" ambayo inahamasisha utekelezaji wa malengo saba ya Mkakati wa Sendai katika kipindi
cha miaka saba. Lengo la mwaka huu linazingatia Kuzuia, Kulinda na Kupunguza idadi
ya watu wanaoathirika
na majanga, ambalo ni Lengo la pili. Lengo
hili linahusu usalama wa watu wote lakini hasa wale walio katika hatari
zaidi ya kifo, kuumia, kuathirika kiafya, madhara ya mfumo wa maisha, kuhama
makazi yao na ukosefu wa upatikanaji wa huduma za msingi kutokana na matukio
ya maafa hasa kwa wanawake, watoto, watu
wenye ulemavu na wazee.
Ikumbukwe katika nchi yetu tuna idadi kubwa ya wananchi walio katika makundi haya.
Takwimu zetu zinaonesha idadi ya wazee ni asilimia 5.5, watoto chini ya miaka mitano ni
asilimia 15.2 na watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ni asilimia
6. Makundi haya ni muhimu na hivyo yanahitaji kuzingatiwa kipekee katika mipango ya usimamizi wa madhara ya maafa.
Ndugu
Wananchi,
Maadhimisho haya yanasisitiza
umuhimu wa nyumba
ya familia kama mahali rasmi na salama wakati wa maafa. Nyumba ya familia
mara nyingi ndipo mahali pa kazi za kujipatia kipato kwa jamii za kipato cha chini hapa nchini. Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanaishi
katika maeneo salama, kwa kuandaa na kutekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi
ya mwaka 1995 na Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 na kutunga na kusimamia
2
utekelezaji wa Sheria ya Mipango
Miji ya mwaka 2007. Vilevile, Serikali imeendelea kuyapanga
na kuyapima maeneo ya makazi ili kuhakikisha wananchi wanaishi
katika makazi bora na salama kuepuka madhara ya maafa. Hadi kufikia Septemba 2017 jumla ya viwanja takriban 3,500,000 vilikuwa vimepangwa na kati ya hivyo takriban viwanja 1,500,000
vimepimwa katika Halmashauri mbalimbali nchini. Vilevile,
ili kupunguza ujenzi holela
na katika maeneo
hatarishi, Serikali imeendelea kuandaa Mipango
kabambe itakayoongoza uendelezaji na ukuaji wa miji. Hadi Septemba 2017 jumla ya Halmashauri 13 zilikuwa katika hatua mbalimbali za uandaaji wa mipango
kabambe.
Ndugu
Wananchi,
Kwa kuelewa umuhimu
wa nyumba ya familia, Serikali imeendelea kuwalinda wananchi
kutokana na madhara
ya maafa kwa kuimarisha mazingira yao na kuwahamishia katika maeneo ya makazi bora. Miongoni mwa hatua hizi ni ukarabati wa tuta la mto Mkondoa
Wilayani Kilosa baada ya kuharibiwa na mafuriko yaliyotokea mwezi
Desemba, 2009 na Januari, 2010 ambapo kaya 5,981 zilikosa makazi.
Vilevile, Serikali iliwapatia wananchi
viwanja katika
eneo la Mabwepande baada ya kuathiriwa na mafuriko katika eneo la Bonde la
Jangwani mwezi Desemba, 2011 ili waishi katika eneo salama. Nasisitiza
Serikali za Mitaa ziongeze kasi ya kupima viwanja ili wananchi wakihitaji kujenga wapate maeneo salama. Aidha, Serikali
ya Awamu ya Tano imendelea kuhakikisha kwamba maeneo yaliyojengwa kiholela yanarasimishwa kwa kupangwa, kupimwa na kuwekewa miundombinu pamoja na kutengewa maeneo ya huduma za jamii katika
3
Halmashauri
mbalimbali. Nyumba zilizojengwa
katika maeneo hatarishi kama vile mabondeni na kwenye
miteremko mikali hayafanyiwi urasimishaji. Vilevile, shughuli za ujenzi zifanyike kwa kutumia
wataalam waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Mjaengo na Wakadiriaji
Majanzi, ambao hadi mwezi Juni 2017 Bodi imesajili wataalam 1,315 na makampuni 354.
Ndugu
Wananchi,
Maafa yanayotokana na matukio yanayohusiana na hali ya hewa
yanaongezeka na kusababisha idadi kubwa ya vifo. Vilevile, takwimu zinaonesha zaidi ya nusu ya vifo vya maafa duniani husababishwa na
matukio makubwa ya maafa ya kijiolojia,
hasa tetemeko la ardhi. Hapa nchini, jumla ya wananchi wapatao 117,721 waliathirika kutokana na
tetemeko la ardhi Mkoani Kagera tarehe 10 Septemba, 2016 na
kusababisha uharibifu wa nyumba za makazi, vifo na majeruhi. Serikali
ya Awamu ya Tano inaendelea na juhudi za kuhakikisha inarejesha hali kwa ubora zaidi na huduma muhimu
kwa wananchi walioathirika.
Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania inakusudia
kusimika vituo vya kuratibu matetemeko ya ardhi katika maeneo ya mkoa wa Kagera ambao kwa sasa unakumbwa na matetemeko ya ardhi ya
mara kwa mara. Mpaka sasa Serikali
kupitia Wakala imesimika jumla
ya vituo tisa (9) vya kudumu vya kuratibu matetemeko ya ardhi ambavyo viko katika maeneo
ya Dodoma mjini,
Kondoa mjini, Kibaya mjini, Singida mjini, Mtwara
mjini, Geita mjini,
Arusha mjini, Mbeya (eneo la gereza la Songwe) na Babati
mjini.
Mafanikio
ya utekelezaji wa Mkakati wa Sendai ni muhimu katika
kufikia Agenda ya 2030 ya Maendeleo
Endelevu, hasa Malengo ya
Maendeleo Endelevu
na Mkataba wa Paris
kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Serikali itaendelea kuzingatia masuala haya na upunguzaji wa madhara
ya maafa katika
utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo
ya Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Pamoja na juhudi za Serikali, nitoe wito, Sisi sote tunawajibika, na mafanikio ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu yanatutegemea.
Ndugu
Wananchi,
Ni dhahiri kwamba kuchukua hatua katika suala hili kutaonesha
kwamba kuna mikakati katika ngazi ya taifa na serikali za mitaa inayolenga usimamizi wa maafa hapa nchini. Suala hili ni changamoto kubwa ambayo inaweza kufanikiwa endapo kutakuwa na ushirikiano
na uratibu mzuri baina ya wadau mbalimbali. Serikali inafanya
marejeo ya Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2004 na kufanya
tathmini na kuandaa ramani kuonesha
maeneo hatarishi kwa majanga ili kusaidia katika kuhakikisha
wananchi wanaishi maeneo salama.
Hivyo nitoe rai kwa Jamii, Wizara, Idara na Taasisi za Umma, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo
kuunga mkono jitihada
za Serikali ya
Awamu
ya Tano katika kuhakikisha wananchi wanaishi
katika mazingira salama dhidi ya madhara
ya majanga mbalimbali. Kwa
ushirikiano wa pamoja, tutakuwa tumefanikisha kuwa na Makazi
5
Salama na kujenga mwamko kwa jamii kuhusu kuchukua hatua stahiki kwa kutambua kuwa maafa hutokea wakati wowote.
“Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi, Punguza Kuhama
kutokana na Maafa”
AHSANTENI SANA
KASSIM MAJALIWA MAJALIWA
WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment