ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 27, 2017

WADAU WA TASNIA YA FILAMU JITOKEZENI KUCHANGIA KATIKA MFUKO WA MAENDELEO YA FILAMU KUSAIDIA KUINUA VIPAJI – MHE. MWAKYEMBE

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Katibu Mfuko wa Maendeleo ya Filamu Bibi. Asha Mtwangi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea taarifa ya hatua iliyofikia mfuko wa maendeleo ya filamu kutoka kwa Katibu wa mfuko huo Bibi. Asha Mtwangi wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Mfuko wa maendeleo ya filamu Bw. Juma Chikoka (kulia) akichangia mada wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu baada ya kikao kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wanatasnia ya filamu nchini kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko wa maendeleo ya filamu ulioanzishwa kwa ajijli ya kukusanya pesa na kutoa mikopo kwa wasanii wa filamu ili kuendeleza vipaji vya filamu nchini.
Hayo ameyasema Jana Jijjini Dar es Salaam alipokutana na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu pamoja na viongozi wa shirikisho la filamu kuzungumza namna mfuko huo utakavyofanya kazi na kulenga makundi yote ya wanatasnia katika mikoa yote nchini.
“Wazo la kuanzisha mfuko huu ni hatua kubwa mno mmechukua pamoja na kujiamini kwani tatizo kubwa tulilonalo linalokwamisha maendeleo ya filamu ni pamoja na ukosefu wa mitajji hivyo kuwaingiza vijana wetu katika mikataba ya unyonyaji; naamini mfuko huu utaondoa kero hiyo na kuboresha maslahi ya tasnia ya filamu nchini” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa atahakikisha kuwa anapitia mikataba ya wasanii wote ili kuona kama mikataba wanayoingia kuandaa filamu inaendana na kazi wanazozitoa kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia wasanii kujitambua na kuingiza kipato halali kitakachoendana na kazi walizofanya.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekosa fursa ya kuonyesha vipaji vyao kutokana na ukosefu wa mitaji au njia elekezi ya kufanisi vipaji vyao, hivyo mfuko wa Maendeleo ya filamu unalenga kuwafikia wasanii wote kutoka mikoa yote nchini kwani ajira kwenye filamu haina ukomo wa umri.
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amempongeza Mhe. Mwakyembe kwa jitihada anazozionyesha katika kupigania maslahi ya wasanii na kuahidi kuwahamasisha wanachama wa shirikisho la filamu kuchangia katika mfuko wa maendeleo ya filamu ili waweze kuinua vipaji na kuleta mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu.

No comments: