ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 16, 2017

WASHINDI WA PROMOSHENI YA COCA-COLA WAJISHINDIA PIKIPIKI

Washindi wa zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya Coca-Cola ya Mchongo chini ya kizibo wakifurahi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
 Meneja usambazaji wa Coca-Cola Mwanza, Samwel Makenge akikabidhi pikipiki kwa baadhi ya washindi wa promosheni ya mchongo chini ya Kizibo inayoendelea katika mikoa ya kanda ya ziwa. ---


Promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’iliyozinduliwa na Coca-Cola mkoani Mwanza hivi karibuni inazidi kuibua washindi ambapo wakazi watatu wa jijini Mwanza wamejishindia Pikipiki na wengine wanaendelea kujishindia televisheni na zawadi mbalimbali.

Promosheni hii inahusisha vinywaji vya Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida na inafanyika mkoani Mwanza na mikoa mingine ya kanda ya ziwa ikiwemo mikoa jirani yake ya Shinyanga na Kigoma na itawawezesha wateja kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi,alisema lengo la promosheni hii kubwa ni kuwazawadia na kuwashukuru wateja wanaotumia bidhaa za kampuni.

“Tumewaletea promosheni hii kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu wote wanaotumia bidhaa zetu kama mnavyoona leo washindi wa promosheni hii wamekabidhiwa zawadi zao,natoa wito kwa wananchi kuzidi kuichangamkia ili kujishindia zawadi kwa kuwa bado kuna zawadi nyingi za kushinda”alisema Kisusi.

Mmoja wa washindi wa Pikipiki,TV, Almes Issa, mkazi wa kitongoji cha Mkuyuni akiongea kwa furaha alisema kuwa hakuamini macho yake baada ya kunywa soda ya Coca-Cola na kufanikiwa kukusanya vizibo vinavyowezesha kupata zawadi ya Pikipiki “Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi ambavyo nimeweza kukabidhiwa zawadi yangu kwa haraka,natoa wito kwa wakazi wa Mwanza tuchangamkie promosheni hii tuweze kujishindia zawadi kama nilivyoshinda mimi”alisema.

Naye mkazi wa Misungwi, Augustino Juma,ambaye ameshinda Pikipiki alisema kuwa kwa ushindi aliopata maisha yake yamebadilika kwa kuwa ataitumia katika shughuli za biashara ya ‘bodaboda’kwa ajili ya kuogeza kipato cha familia.

Washindi wengine waliokabidhiwa zawadi mwishoni mwa wiki ni Lucas Gwanjingi aliyejishidia pikipiki,Maria Simon aliyejishindia TV na Enock Matusera aliyejishindia T shirt ya Coca-Cola.

Kisusi, alisisitiza kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.

Alisema zawadi zote kubwa zitatolewa kwa washindi kiwandani na zawadi ndogondogo zitatolewa kwa mawakala wanaouza bidhaa za kampuni na magari ya usambazaji vinywaji vya Coca-Cola.

No comments: