ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 28, 2017

WAZIRI MPINA ACHOMA NYAVU KUKOMESHA UVUVI HARAMU

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akimimina mafuta ya taa kabla ya zoezi la kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu mjini Kigoma leo. Nyuma yake ni baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma watumishi wa umma na wanahabari wakishuhudia tukio hilo.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma leo.
 Nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zenye dhamani ya shilingi milioni 31 zikiteketea kwa moto kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu nchini.

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika serikali hii ya awamu ya tano.
Akiongea mara baada ya kuteketeza nyavu hizo hizo mapema leo, Mpina alionyesha kushangazwa na suala la uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita hii haina mwisho? Lazima yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha zinazotumika ni duni, ifike mahala suala hili  liwe historia”. Alisema Mpina.
Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito.
“kama nitashindwa kushughulia suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa wamejuruhiwa.” Alisisitiza Mpina.
Akiwa katika ziara ya Oparesheni Maalum ya Ondoa Mifugo kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani akiwemo Mkoani kigoma, Mpina Pia alitembea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa kugandisha barafu inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi mwaloni hapo pamoja na suala la kuwauzia dagaa wafanya biashara wanaozisafirisha nje ya nchi. Waziri Mpina Pia alitembelea chuo uvuvi mjini Kigoma.
Zoezi la opareshini ondoa mifugo na kukomesha rasmi uvuvi haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara husika wakiongozwa na mawaziri Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia kazini katika mikoa inayokabiliwa na changamoto hizo. 

No comments: