Advertisements

Wednesday, October 18, 2017

ZIMAMOTO WAKONGA NYOYO ZA WANANCHI MAONESHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

 Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji toka Makao Makuu, Damian Muheya (Kulia), akiwaelimisha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jinsi vizimia moto vya awali (Fire Extinguisher) vinavyotumika pindi moto unapotokea, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
 Wananchi wa Mjini Kilimanjaro wakiwa katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakipata elimu juu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye vyombo vya Usafiri na Usafirishaji, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”.
 Wananchi wa Mjini Kilimanjaro wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kitengo cha Maokozi Saidi Seng’endo (Kushoto) walipotembelea banda hilo, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. 
 Picha ni sehemu ya mabanda ya washiriki mbalimbali wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”.
 Picha watoto wakimsikiliza Konstebo Saidi Seng’endo juu ya matumizi ya kifaa kinachohifadhi hewa safi (Breathing Apparatus) kwa ajili ya kumsaidizi Askari wa Zimamoto kwenye matukio mbalimbali.
Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu, Saidi Seng’endo (Kushoto), akiwa na Konstebo wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Simba Mikidadi (Kulia), wakiwaonesha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro jinsi baadhi ya vifaa vya gari maalum la maokozi  (Fire Rescue Tender) vinavyotumika pindi ajali inapotokea barabarani, wakati wa Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayoendelea Mkoani humo katika viwanja vya Mashujaa, ikiwa yameingia siku ya tatu tangu kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu, tarehe 16/10/2017. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “ZUI AJALI, TII SHERIA, OKOA MAISHA”. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

No comments: