Naibu waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi kuacha dhana potofu kuwa kingatiba za matende na mabusha zina madhara.
Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji wa mabusha na ngirikokoto(henia) kwa wananchi 200 ambapo zoezi hili limedhafadhiliwa na kampuni ya utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi ya Statoil mjini hapa
Naibu waziri afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt.Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa mkoa wa Lindi kuacha dhana potofu kuwa kingatiba za matende na mabusha zina madhara
Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji wa mabusha na ngirikokoto(henia) kwa wananchi 200 ambapo zoezi hili limedhafadhiliwa na kampuni ya utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi ya Statoil mjini hapa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile(wa pili kulia) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 264 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Statoil, Bw. Oyotein Michelsen. Fedha hizo ni kwa ajili ya kambi za upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa watu wapatao 400 kwa mwaka 2017 na 2018.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akihutubia wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa upasuaji wa mabusha na ngirikokoto kwa wagonjwa wapatao 200 wa Manispaa ya Lindi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akipokea mashine ambayo ina kisu cha moto ambacho kinazuia damu wakati wa upasuaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Statoil.
Mkurugenzi wa Statoil, Bw.Oyotein Michelsen akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa kambi ya upasuaji inayofanyila kwenye hospitali ya rufaa ya Sokoine mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment