ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 23, 2017

MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA YADHIBITIWE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selamani Jafo akifungua kongamano ya Chama cha Wahasibu Tanzania  linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa linalofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa Kongamano linalohusu uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Washiriki na wajumbe wa chama cha Wahasibu Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Ufunguzi wa Kongamano lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Mhe.Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania Fred Msemwa wakati wa Ufunguzi wa Kongamano linalofanyika Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo(Katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wahasaibu Tanzania pamoja na wawwezeshaji wa Kongamano hilo.

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo  amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima kwenye Halmashauri ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa kongamano la siku mbili la Chama cha Wahasibu Tanzania(TAA) lililojumuisha wataalam wa Hesabu na wafanya maamuzi kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Katika Kongamano hilo ambalo Linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Chama hicho mwaka 1983 limelenga kujenga uwezo kuhusu Uwazi na Uwajibikaji kwa Viongozi waandamizi wa Mamlaka ta Serikali za Mitaa katika Matumizi ya Fedha za Umma.

Waziri Jafo amesema kuwa Bajeti kubwa ya Serikali inapelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa takribani asilimia 20.7 ya Bajeti ya Serikali huelekezwa katoka Halmashauri hivyo ni eneo ambalo linapata  Fedha nyingi na zinahitajo uangalizi mkubwa.

Tunafahamu kuwa Viongozi wa Halmashauri mna Mamlaka kamili ya kupanga matumizi ya Fedha hizo lakini angalieni maeneo ambayo yataleta Tija kwa Wananchi na yatatatua changamoto zinazowaathiri wananchi wetu katika maisha yao ya kila siku, huko ndio sehemu ya kutumia  Fedha nyingi na si vinginevyo.

Katika maeneo ambayo hayanipi amani na bado nayaona kuwa na matumizi mabaya ya Fedha ni eneo la Manunuzi ya Umma nawasihi muwaelimisha vya Kutosha viongozi hawa namna ya kudhibiti mianya yote ya Upotevu wa Fedha uliopo katika eneo la Manunuzi"
Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa kuna tabia ya kubadilisha matumizi ya vifungu"Realocation" bila sababu za Msingi na bila kufuata taratibu zinazohitajika suala hili limekua likisababisha hoja nyingi wakati wa Ukaguzi wa Hesabu nawasili viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa mkaliangalie hilo kwa jicho la tati na mkalidhibiti.

Akitoa neno la Ufunguzi Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzani  Fred Msemwa amesema Chama hiki kina umri wa Miaka 34 na kina lengo la kuendeleza Taaluma za Uhasibu Tanzania na kutoa elimu ya Fedha na Biashara kwa wananchi ili waweze kujisimamia katika mapato na matumizi yao.

Msema alisema kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya Kodi, Ongezeko la Thamani,sheria za Fedha na mabadiliko yake pamoja na kuanzisha Dawati la Mhasibu ambalo hutoa uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya Fedha, biashara na Rasilimali.

Kongamano hili ni endelevu na litakua likifanyika kila mwaka  na litakuwa likiwajengewa uwezo viongozi wa Serikali ambao wengine hawana utaalam wa Uhasibu namna ya kuipitia kwa umakini taarifa ya Mkaguzi wa Ndani, viashiria vya Rushwa katika matumizi ya Fedha za Umma, kuzuia vihatarishi, namna ya kuongeza vyanzo vya mapato na namna ya kupata Fedha za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

No comments: