Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew
Masawe (katikati), wakishuhudia uchukuliwaji wa alama za vidole za mmoja wa
wananchi waliofika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, mkoani Mara
kuandikishwa kwa ajili ya kupata kitambulisho cha utaifa. Kupitia zoezi hilo
wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vya
Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akiingiza taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa, baada ya kuzindua zoezi
la usajili wa vitambulisho hivyo leo Mkoani Mara.Kupitia zoezi hilo wananchi wa
mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vinavyotolewa na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akiakisi fomu ya taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa, baada ya
kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho hivyo leo Mkoani Mara.Kupitia zoezi
hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho
vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala na Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Masawe
(kulia),wakiteta jambo baada ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), kuzindua zoezi la usajili wa
vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi
Mkendo,mkoani Mara.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa tayari
kuhudumia wananchi waliofika katika zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa
baada ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), katika Viwanja vya Shule ya
Msingi Mkendo,mkoani Mara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment