Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora Mkemwa.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akizungumza jambo alipotembelewa na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda akizungumza jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda alipomtembelea Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula(kushoto) wakimuonyesha Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi kifungu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kinachozungumzia utoaji wa huduma za jamii alipotembelea Ofisi za Naibu Waziri wa huyo leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri
Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL
Mahruqi (wa pili kutoka kulia) alipotembelea Ofisi za TAMISEMI Jijini Dar es
Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora
Mkemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya
Bibi. Zainabu Chaula pamoja na mmoja wa Afisa kutoka Mambo ya Nje ya Nchi Bw.
Odiro. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)
Na
Eliphace Marwa
BALOZI
wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na na
hatua mbalimbali znazochuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga
mazingira bora kwa wawekezaji na wengi wao wapo mbioni kuja kuwekeza katika
miradi mikubwa ya maendeleo nchini.
Balozi Al Mahruqi
aliyasema hayo leo aJijini Dar es Salaam wa mazungumzo baina yake na Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph
Kakunda na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo
Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Mahruqi alisema
miongoni mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini
ni pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo
upatikanaji wa tasnia ya nyama.
“Serikali ya Oman ina
mpango wa kuja kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kipaumbele kikubwa
kitakuwa ni nchi ya Tanzania kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo
Tanzania,” alisema Balozi Mahruqi.
Aidha Balozi Mahruqi
aliitaka Serikali kuharakisha makubaliano ya mikataba baina ya Mataifa hay ili kuwezesha
wawekezaji kutoka Oman kupata fursa ya kuwekeza nchini na kuweka mazingira
rafiki kwa wawekezaji kutoka Oman.
Kwa upande wake Naye Naibu
Waziri Kakunda alimuahidi Balozi Mahruqi
kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman
wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji
yao.
“Nitafuatilia kwa
kina kwa wataalamu weu wanaohusika na uwekezaji kwenye kiwanda cha nyama ambapo
wawekezaji kutoka Oman watawekeza takribani dola milioni tatu ambazo zitasaidia
wafugaji wa Watanzania kupata soko la mifugo yao” alisema Naibu Waziri Kakunda.
Aidha Kakunda aliahidi
kufuatilia maeneo ambayo Serikali ya Oman iliahidi kusaidia kaika ujenzi wa
visima mia moja vya maji katika maeneo ya mashule ili kupata orodha kamili ya
shule zinazotakiwa kupatiwa msaada huo.
No comments:
Post a Comment