Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuhusu kuwepo kwa nafasi
wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia, Lazaro Samwel
Nyalandu kujivua Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo
kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.
Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania
ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya
Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo, Onesmo Ole Nangole
alikuwa ni Mbunge.
Wakati huo huo Waziri wa Tamisemi kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini
ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,
ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano
zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
Hata hivyo, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi
Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi
itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata
hizo hapo baadae.
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo
Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
NA. | MKOA | HALMASHAURI | JIMBO |
1. | Singida | Halmashauri ya Wilaya ya Singida | Singida Kaskazini |
2. | Arusha | Halmashauri ya Wilaya ya Longido | Longido |
Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
NA. | MKOA | NA. | HALMASHAURI | NA. | KATA |
1. | Kagera | 1. | Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. | 1 | Keza |
2. | Arusha | 2 | Halmashauri ya Jiji la Arusha | 2 | Kimandolu |
3. | Pwani | 3. | Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. | 3 | Kurui |
4. | Tabora | 4. | Halmashauri ya Wilaya ya Tabora | 4 | Bukumbi |
5. | Tanga | 5. | Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe. | 5 | Kwagunda |
Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
16 NOVEMBA, 2017
No comments:
Post a Comment