Wananchi wa Zimbabwe waliojawa na
furaha wameandamana katika Jiji la Harare wakishinikiza rais Robert
Mugabe ajiuzulu.
Waandamanaji hao wameonekana
wakiwakumbatia wanajeshi kuwapongeza kwa uamuzi wa kuchukuwa udhibiti
wa nchi hiyo tangu jumatano.
Maandamano hayo yanaungwa mkono na
wanajeshi na wanachama wa chama tawala wa Zanu-PF, huku maveterani wa
vita nao wakimtaka Mugabe aachie madaraka.
Waandamanaji wakiwa na picha za Mkuu wa Majeshi Jenerali Constatino Chiwenga pamoja na Makamu wa Rais Emerson Mnangagwa katika kuwapongeza
No comments:
Post a Comment