Advertisements

Wednesday, December 27, 2017

Kura za Urais zaanza kuhesabiwa nchini Liberia

Shughuli ya kuhesabu kura imeanza nchini Liberia kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais. Uchaguzi huo utaamua ni nani atakuwa Rais mpya wa Liberia kati ya mwanasoka wa zamani George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boakai.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Liberia, Jerome Korkoya amesema matokeo rasmi yanatarajiwa katika kipindi cha siku chache zijazo.
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 70, taifa hilo la magharibi mwa Afrika litashuhudia Serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ikikabidhi madaraka kwa nyingine.
Duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa rais ilicheleweshwa baada ya kesi kuwasilishwa katika mahakama ya juu kupinga kufanyika kwa kura hiyo kwa madai ya kuwepo udanganyifu wa kura katika duru ya kwanza.

Chanzo: Mwananchi

No comments: