Advertisements

Thursday, December 28, 2017

MWANASOKA GEORGE WEAH ASHINDA URAIS WA LIBERIA

ALIYEWAHI kuwa mcheza soka bora duniani, George Opong Weah, ameshinda katika uchaguzi na kuwa Rais wa Liberia baada ya kushinda katika wilaya 12 miongoni mwa 15 zilizomo katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.

Weah ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuwashukuru watu wote waliompigia kura akisema mipango yake ni kuleta ukombozi kwa nchi nzima.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya AC Milan ya Italia, anakuwa rais wa 25 wa nchi hiyo ambapo aliyekuwa makamu wa rais kwa miaka 12 iliyopita, Joseph Boakai, alipata ushindi katika wilaya mbili tu.

No comments: