Washiriki wa shindano la Avance Media kwa Watanzania 50 wenye umri mdogo na wenye ushawishi kwa mwaka 2017 wametajwa.
Watanzania hao 50 huchaguliwa kwa kupigiwa kura wakitokea katika sekta mbalimbali kama vile biashara, burudani, Sheria na utawala, sekta ya habari, sayansi na teknalojia, michezo, uwajibikaji katika jamii na kujitolea.
Kwa mujibu wa waandaji wa shindano hilo, washindi watatangazwa tarehe 16 mwezi January mwaka 2018
Ikiwa ni moja ya mashindano yenye heshima kubwa, shindano hili hutoa mchango wa kipekee kwa kutambua jitihada mbali mbali zinazofanywa na Watanzania wenye umri mdogo katika sekta mbali mbali
Mkurugenzi Mtendaji wa Avance Media, Prince Akpah alisema “Kwa mwaka huu, Mtanzania mwenye ushawishi Zaidi ni yule ambaye kazi yake pasipo na shaka imekuwa na mchango chanya kwa maisha ya Watanzania. Washiriki wote waliotajwa na wanaoshiriki, wamerweza kuvuka kigezo cha kufanya kazi kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wengine kupitia kujituma, kufanya kazi kwa bidii ,kujitolea na kibubwa Zaidi kufanya maamuzi ya kijasiri,”
Pazia la upigaji kura tayari limeshafunguliwa kupitia tovuti ya tz.avancemedia.org ili kuweza kumpata mshindi mmoja mwenye ushawishi aidi katika sekta nane ambazo zitapigiwa kura
Zoezi hili pia linafanyika katika nchi za Cameroon, Ghana, Nigeria, South Africa, DR Congo na Kenya.
Washiriki waliotajwa ni wafuatao
Kwenye biashara (kwa kushirikiana na TANOE Business)
- Carol Ndosi (Alta Vista Events)
- Harun Elias (Javis International Trade Co.)
- Hellen Dausen (Nuya's Essence)
- Ian Ferrao (Vodacom Tanzania)
- Krantz Mwantepele (KONCEPT)
- Patrick Ngowi (Helvetic Solar)
- Yusuf Bakhresa (Azam Media Ltd)
Burudani (kwa kushirikiana na WatsUp TV)
- Ali Kiba (mwanamuziki)
- Diamond Platinumz (mwanamuziki)
- Jokate Mwegelo (muigizaji)
- Joti (mchekeshaji)
- Riyama Ally (mwigizaji)
- Vanessa Mdee (mwanamuziki)
- Wema Sepetu (mwigizaji)
Sheria na Utawala
-
- Benedict Ishabakaki (mwanasheria)
- Bonnah Kaluwa Mbunge)
- Fatma Karume (mwanasheria)
- Jebra Kambole (mwanasheria)
- Peter Kibatala (mwanasheria)
Maisha
- Benjamin Fernandes (Mwendesha kipindi cha Tv)
- Flaviana Matata (mwanamitindo)
-
Jacqueline N Mengi (mwanamitindo)
- Millen Magese (mwanamitindo)
- Miriam Odemba (mwanamitindo)
- Osse Greca Sinare (mpiga picha)
Tasnia ya Habari
- Babbie Kabae (Clouds 360)
- Bdozen (Clouds Media)
- Dina Marios (E-FM Radio)
- Idris Sultan (SIO HABARI)
- Millard Ayo (Ayo TV)
- Salim Kikeke (BBC Swahili)
Sayansi na Teknolojia
- Edwin Bruno (Smart Codes)
- Evans Makundi (EvMak Tanzania Ltd)
- Fayaz Valli (GetCore Group)
- Johnpaul Barretto (Kinu Innovation Space)
- Jumanne Mtambalike (Sahara Ventures)
- Lilian Makoi (Jamii Africa )
Michezo
-
Hashim Thabit Manka (Yokohama B-Corsairs)
- Juma Kaseja (Young Africans SC)
- Mbwana Samatta (KRC Genk)
- Mrisho Ngasa (Fanja SC)
- Shomari Kapombe (Simba SC)
- Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna)
- Faraja Nyalandu (Shule Direct)
- Irene Kiwia (Tanzania Women of Achievement)
- Jennifer Richard Shigoli (Tanzania Netherland Vocational Training Center)
- Nancy Sumari (The Neghesti-Sumari Foundation)
- Rebeca Gyumi (Msichana Initiative)
- Saira Dewji (Mo Dewji Foundation)
Shindano hili huandaliwa na Avance Media kwa kushirikiana na BioPlus, ReputationPoll.com, Abjel Communications, WatsUp TV, YCEO, TANOEBusiness.com, My Naija Naira, Dream Ambassadors Foundation GH, CliqAfrica na CELBMD Africa.
No comments:
Post a Comment