Advertisements

Thursday, December 28, 2017

Obrey Chirwa azua gumzo kuhamia shambani Zambia

Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa 

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amezua gumzo mtandaoni baada ya kutuma picha kwenye mtandao wake wa Istangram akiwa shambani.

Mzambia huyo alionekana kwenye picha akiwa shambani akipalilia mahindi huku akiwa ameshika jembe la mkono.

Inaelezwa kwamba huenda mchezaji huyo yupo kwenye mapumziko, lakini akisubiri kumaliziwa fedha zake za usajili.

Awali Chirwa aliuomba uongozi wa Yanga kummalizia kumlipa fedha zake ndipo atakarudi nchini kuendelea na kazi yake ya kusakata soka.

Yanga inatarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu mchezo unaotarajiwa kupigwa tarehe Jumapili wiki hii jijini Mwanza.

MWANASPOTI

No comments: