Advertisements

Thursday, December 28, 2017

Winga Mtanzania anayekipiga Marekani afikiria soka la Ulaya

Mchezaji Mtanzania anayecheza soka Marekani,
By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Winga wa Mtanzania, Daud Aboud (18) anayekipiga LCC Mean's Soccer ya Marekani amesema hakuwahi kujutia kujihusisha na mchezo wa mpira wa miguu.

Winga huyo mwenye uwezo wa kucheza pande zote mbili kushoto na kulia, alitembelea jana Jumanne ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) zilizopo Tabata Relini jijini hapa.

Aboud alisema ni matarajio yake kucheza soka Ulaya na mwezi ujao anatarajia kujiunga na timu mpya ambapo mipango ikikamilika ataweka wazi.

Kinda huyo alisema, "Changamoto zilizopo kwenye soka ni nyingi lakini sijawahi kabisa kuwaza kuachana na soka kwani linaweza kuleta kila kitu zikiwemo fedha," alisema kinda huyo.

Hata hivyo Aboud aliishukuru kampuni ya Mwananchi kwa kuwa pamoja naye katika utafutaji wa maisha yake ya soka.

"Nipo kwa mapumziko mafupi ila niliona ni vizuri kuja kuwatembelea, Marekani pamenijenga kuelekea kwenye ndoto zangu zangu," alisema Aboud.

MWANASPOTI

No comments: