Advertisements

Wednesday, December 27, 2017

SERIKALI YAANZA KUWASHUGHULIKIA WASANII WANAOVAA NUSU UCHI

Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania.

Waziri Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika.

"Pale tunapoona kuna ukiukwaji, tufumbe macho tusijali malalamiko yanavyokuja kutolewa, maana ukiwagusa wasanii walikuwa wanakuja juu sana, lakini tunashukuru mkuu wa nchi kulisemea hilo, basi na sisi tumeongezewa nguvu basi hatutaachia suala hilo kuendelea kuharibu vizazi vyetu", amesema Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho.

1 comment:

Anonymous said...

Bongo tuache MAMBO YA KALE. Mambo yanaenda na wakati. It is all about Art. 21th century art trends ni tofauti. Kazi za Wasanii lazima zikidhi International Market, ama sivyo hawatatambulika kimataifa, na hilo siyo jambo jema kiuchumi. Sidhani kama Mheshimiwa Rais na Waziri Mwakyembe wataweza kupromoti Wasanii wetu kimataifa, kama wakuwa na hii old philosophy. Besides, nadhani URais unao majukumu muhimu zaidi kuliko hili. A common man or woman doesn't see this as a pressing issue. Watu wanataka maendeleo ya kiuchumi...and that is what we voted for you President Magufuli. Cultural issues zisikupotezee muda, hata kama utakaa miaka mia moja hutaweza kuzitatua because, the world is changing by day and night. After all, hawa wasanii wanatafuta ridhiki, na hilo ni jambo nzuri. Tafadhali Waziri Mwakyembe, jaribu kutumia elimu yako kama mwanasheria kumshauri Rais, kwa vile hakuna faida yeyote itakayopatikana katika ku -censor Artistic expressions nchini. Mawaziri inabidi muwe advisors wa Rais, kuna mengi Rais hayajui, hivyo ni jukumu lenu kumsaidia badala ya kuwa "YES SIR" kwa kila kitu anachowaambia.