Advertisements

Wednesday, December 27, 2017

CCM yamjibu Askofu Kakobe baada ya kuikashifu serikali

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la FGBF lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam amekosa hekima na busara kwa kugeuza madhabahu ya kanisa kuwa jukwaa la kisiasa na kuanza kukashifu viongozi wa serikali akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Frank Kamugisha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Aksofu Kakobe kukosoa namna serikali inavyotenda mambo yake, akisisitiza kwamba Tanzania si nchi ya chama kimoja kama ambavyo viongozi wanataka kuigeuza na hivyo kuwataka viongozi wa serikali waanze kutubu.

Kamugisha amesema kuwa, wao kama viongozi wa CCM hawaweza wakakaa kimya wanapoona chama kinachafuliwa na viongozi wake ambao wanafanya kazi kwa niaba ya watanzania wakikashifiwa.

Aidha, alisema kuwa, siasa ni kwa ajili ya wanasiasa, na kama kiongozi wa dini ana jambo lolote analotaka kuzungumzia, kuna busara za kutumia na sio kutumia kanisa kusema hayo.

No comments: