Advertisements

Thursday, January 18, 2018

Dr. Mashinji Akanusha Kuugua Ghafla na Kupelekwa Amana

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Vincent Mashinji  amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa, ni mgonjwa na amelazwa katika Hospitali ya Amana.

Mashinji amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, yupo mzima wa afya na anaendelea na kikao cha Kamati Kuu katika Hoteli ya Bahari Beach. Amesema huenda kuna makosa kwa aliyemhusisha na kikao.

Taarifa hiyo ya uzushi iliyokuwa ikisambaa ilisema;
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Vincent Mashinji, ameugua ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Shani Mwaruka amethibitisha kumpokea Dk. Mashinji leo saa tano asubuhi akiwa mahututi ingawa amesema ni mapema mno kujua kinachomsumbua hadi hapo madaktari watakapotoa ripoti baada ya kumfanyia uchunguzi.


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amefika hospitalini hapo kumjulia hali Dk. Mashinji ambaye amelazwa katika chumba cha dharura.

No comments: