Advertisements

Saturday, January 13, 2018

GEITA WAADHIMISHA SIKU YA MAPINDUZI KWA KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki na wananchi kukusanya mchanga wa kufyatulia tofari ambazo zinatumika kujengea shule ya Sekondari kwenye Kijiji cha Mulanda kata ya Buseresere Wilaya Chato. 
Baadhi ya viongozi wa chama Tawala pamoja na Diwani wa Kata ya Buseresere Godfey Miti wakishiriki kwenye shughuli ya ufayatuaji matofari.
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye shughuli ya uchimbaji wa mchanga wa kujengea madarasa ya shule ya sekondari ambayo ni mpya. 
Diwani wa Kata ya Buseresere, Godfrey Miti akielezea namna ambavyo wananchi wameguswa kushiriki ujenzi wa shule kijiji cha Mulanda. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikusanya michango kutoka kwa wadau mbali mbali wa maendeleo ambao walikuwa wamejitolea kuchangia ujenzi wa shule hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Robert Luhumbi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wakiwemo na viongozi .

Na Joel Maduka, Chato.
Ikiwa Tanzania imeadhimisha miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar ,serikali Mkoani Geita imetumia siku hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa Mulanda Kata ya Buseresere kufanya shughuli za maendeleo za ujenzi wa shule ya sekondari kijijini hapo.

Ujenzi huo ambao umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi kwa kushirikiana na wanakijiji wa kijiji hicho umetokana na adha ambazo wamekuwa wakizipata wanafunzi ambao wanasoma shule ya sekondari ya Buseresere ambao wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita sita kufuata elimu.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Buseresere,Godfrey Miti ,alisema maamuzi hayo ambayo yalichukuliwa na wananchi yametokana na kwamba kata hiyo inawananchi wengi na kwamba shule iliyopo ilikuwa haitosho kutokana na kwamba wanafunzi wa kidato cha kwanza 736 ambao wanatarajia kusoma kwenye shule ya kata hali ambayo inaonesha kuwepo kwa wanafunzi wengi zaidi na kwamba kukamilika kwa shule hiyo itasaidia kupunguza wingi wa wanafunzi kwenye shule ya sekondari Buseresere.

Aidha kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi,aliwataka wananchi kutambua kuwa akuna mgeni ambaye anaweza kuleta maendeleo na kwamba maendeleo yanaitaji kuwa na mapinduzi ya kifikila huku akiwashukuru wananchi kujitoa kwenye ujenzi wa shule hiyo.

Mhandisi,Luhumbi ameongezea kuwa matarajio ni kuona ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018 kila kijiji kinakuwa na zahahati ili kuhepukana na usumbufu wa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi yaliyoshuhudia kuangushwa kwa utawala wa Sultan na familia yake January 12 mwaka 1964.

Mwaka huu yamefanyika huku Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ikiwa imepiga hatua katika kupambana na umasikini na kuimarisha demokrasia licha ya changamoto kadhaa za kisiasa zinazoendelea kushuhudiwa.

Wazanzibari wanaona siku hii inapaswa kutumiwa na Serikali kujitathmini kuangalia hatua walizopiga na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili Zanzibar.

Zaidi ya wanamapinduzi 800 walishiriki kwenye mapinduzi hayo yaliyoifanya Zanzibar kuwa huru kutoka kwa utawala wa Kisultani.

Sherehe za zimejumuisha vikosi vya ulinzi na usalama sambamba na maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar.

No comments: