Advertisements

Sunday, January 14, 2018

Polisi wamkamata mfanyabiashara akisafirisha mamilioni


By Pamela Chilongola,Mwanachi pchilongola@mananchi.co.tz

Polisi Kitengo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), inamshikilia mfanyabiashara wa vifaa vya magari, Boniface Mbilinyi (32) kwa tuhuma za kusafirisha dola 83,000 za Marekani sawa na Sh182.6 milioni.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 14, 2018, Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha fedha hizo kwenda Dubai.

Amesema polisi walimkamata mfanyabiashara huyo Januari 13 saa 9 alasiri uwanjani hapo kwa kushirikiana na maofisa wa Forodha, kwamba alikuwa akisafiri na dola 123,000 za Marekani.

Amesema kati ya hizo, dola 40,000 za Marekani zilithibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini dola 83,000 za Marekani hakuzitolea taarifa yoyote.

“Tulimkamata akiwa anakaguliwa eneo la ukaguzi wa uwanja huo. Mtuhumiwa tunamshikilia kwa mahojiano zaidi hivyo tunategemea kesho kupeleka jalada kwa Mwanasheria wa Serikali ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema Mbushi.

No comments: