ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 25, 2018

WANANCHI WAZIDI KUJIZOLEA MAMILIONI YA TATUMZUKA,WAZIDI KUNG'ARISHA MAISHA YAO



Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani,mapema jana jijini Dar wakati wa kuwatambulisha washindi wawili wa Tatumzuka waliopatikana mwishoni mwa wiki Jumapili Januari 21 2018, kupitia Mzuka Jackpot ambayo pia ilirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya ITV, Clouds TV na TV1.Pichani kulia ni Mzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27. na kushoto ni Britony Mtalemwa kutoka Songea,ambaye alijishindia milioni 40.
Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka, Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi Ndugu Britony Mtalemwa kutoka Songea,ambaye alijishindia milioni 40.


Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundiMzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27.

Meneja Mawasiliano kampuni ya michezo ya kubahatisha ya TatuMzuka,Sebastian Maganga alisema kuwa wanayo furaha kubwa ya kuwatambulisha washindi wawili wa Tatumzuka waliopatikana tarehe 21 Januari 2018, jumapili iliyopita kupitia Mzuka Jackpot ambayo pia ilirushwa moja kwa moja kupitia vituo vya ITV, Clouds TV na TV1.

Maganga aliwataja washindi hao kuwa ni Mzee Emmanual Shayo kutoka Pugu Dar es Salaam ambaye alijishindia milioni 27,Mshindi mwingine alikuwa ni Britony Mtalemwa ambaye ametokea Songea,ambaye alijishindia milioni 40.

"Washiriki wa wiki hii walichukua jumla ya milioni 134 kwa pamoja. Washindi wengine wa wiki hii walikuwa ni Gibson Erasmas kutoka Mwanza aliyeondoka na milioni 40 na Andrew Kagoma kutoka Arusha aliyejinyakulia milioni 27'alisema Maganga..

Amesema Tatu Mzuka inawawezesha Watanzania wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali na mikoa tofauti kuliko mchezo mwingine wowote. Kama Tatu Mzuka, amini kwamba tunatafuta njia zaidi kukupa fursa ya kuwa milionea kwa kiwango cha chini kabisa cha shilingi 500.Kila saa ndani ya siku, Tatu Mzuka inakupa fursa ya kushinda hadi milioni 6.Kila siku, siku sita za wiki kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi tuna droo ya milioni 10 inayoitwa ‘Mzuka Deile’.

"Na Jumapili ya wiki hii, tuna milioni 60 ambayo inatafutiwa mshindi,Nafasi hizi zote zinapatikana kwako kwa kiasi cha shilingi 500 tu''alimaliza kusema Maganga.

No comments: