Advertisements

Friday, January 19, 2018

WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua chumba cha upasuaji wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Serengeti akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya matibabu ya bure kwa wazee, Johaness Chacha, moja wa wazee 280waliopatiwa vitambulishbo hivyo vitakavyowawezesha kutibiwa bure popote wilayani Serengeti katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya ya Mugumu Januari 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa Mhandisi Andrea Nyantori kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti Januari 18, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee baada ya kuwakabidhi vitambulisho vya kuwawezesha kupatiwa matibabu bure hospitall yoyote wilayani Serengeti. Makabidhiano Hayo yalifanyika kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya Serengeti Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mhandisi, Andrea Nyantori ambaye alichanga shilingi milioni 10 katika harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti katika mji mdogo wa Mugumu, Januari 18, 2018. (Picha cha Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askari Magereza wa gereza la Tabora Moja wilayani Serengeti wakati alipotembela gereza hilo kukagua mradi wa ufugaji ng'ombe wa nyama na maziwa Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wenza wa askari magereza wa gereza la Tabora Moja baada ya kukagua mradi wa ufugaji ng'ombe wa nyama na maziwa katika gereza hilo na kuzungumza na askari Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 18, 2018.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Serengeti, Cha Marwa katika mkutano wa hadhara alipuhutubia kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu wialyani Serengeti Januari 18, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Serengeti, Cha Marwa katika mkutano wa hadhara alipuhutubia kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu wialyani Serengeti Januari 18, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa mji mdogo wa wilaya ya Serengeti wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mbuzi katika mji mdogo wa Mugumu Januari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amegawa kadi za matibabu kwa wazee 280 wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, kadi hizo zitawawezesha wazee hao kutibiwa bure.
Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu bure kwa wazee walio na umri wa kuanzia miaka 60.


Waziri Mkuu alikabidhi kadi hizo jana (Alhamisi, Januari 18, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, inayojengwa katika mji wa Mugumu.


Alisema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti itakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo, itakayokuwa na uwezo wa kuwahudumia wakazi wa wilaya hiyo na wageni.

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muhimu kwa kuwa mbali na kuwanufaisha wananchi, pia watalii wanaotembelea mbuga ya Serengeti nao wataweza kutibiwa hapo.

Awali, Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Nurdin Babu alisema tangu mwaka 1974 wilaya hiyo ilipoanzishwa hadi sasa haina hospitali ya wilaya na wakazi wake wanatibiwa katika hospitali teule ya Nyerere inayomilikiwa na kanisa la Mennonite Tanzania.

Alisema kutokana na kuongeka kwa idadi ya wakazi hao pamoja na idadi kubwa ya wageni wanaotembelea Serengeti, hususan watalii hospitali hiyo haina tena uwezo wa kutoa huduma kwa kiwango kinachostahili.

Bw. Babu alisema mara nyingi wageni wanaotembelea mbuga ya Serengeti hulazimika kufuata huduma za afya mjini Arusha au Nairobi nchini Kenya pale wanapougua au kupata ajali katika shughuli zao za kitalii.

Alisema kwa upande wa wakazi wa wilaya ya Serengeti wao hulazimika kufuata huduma za afya katika hospitali ya Mkoa au hospitali ya Rufaa ya Bugando, hivyo kukamilika kwa mradi huo wa ujenzi wa hospitali utawapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Pia Mkuu huyo wa wilaya alisema alianzisha kampeni ya changia sh. 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya, kwa lengo la kuwafanya wakazi hao wajisikie kuwa wameshiriki katika ujenzi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 19, 2018.

No comments: