ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 28, 2018

BONGO MOVIES SHINYANGA WANAKULETEA FILAMU MPYA 'LAANA YA MKE' ,TAZAMA TRAILER HAPA

Mwaka mmoja baada ya kuachia Filamu ya ‘Nyama ya Ulimi’,Bongo Movies Shinyanga wanakuletea Filamu nyingine kali inaitwa “Laana ya Mke” ambayo itazinduliwa rasmi Machi 23,2018.
Filamu hiyo yenye ubora wa hali ya juu inahusu majanga na laana wanazopata wanaume wababe,wasio na fadhila wanaotafuta mali na wake zao kisha kuwafanyia ukatili.
Katika Filamu hii iliyoongozwa na Director mahiri Dave Skerah wamo Magwiji wa Filamu akiwemo Blandina Chagula ‘Johari’, Ibrahim Songoro ‘Songoro Gadafi’,Magreth Emmanuel, Mariam Bilal, Najma Shahel,Edward Joseph na Mzee Salum Kawelewele.
Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Juma Ibrahim Songoro amesema uzinduzi wa filamu ya Laana ya Mke utafanyika tarehe 23.03.2018 katika ukumbi wa NSSF ya zamani “CCM mkoa wa Shinyanga” kuanzia saa tatu usiku.
TUMIA DAKIKA ZAKO 2 TU KUANGALIA KIONJO CHA FILAMU YA LAANA YA MKE

No comments: