ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 15, 2018

JAPAN YAKABIDHI MRADI WA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA KASENDA WILAYANI CHATO WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 320

 Balozi wa Japan Nchini Tanzania. Yoshida Masaharu pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, bw Joel Hari wakiweka jiwe la makabidhiano ya mradi wa Soko la Kimataifa la Samaki ambalo limefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa Gharama ya Shilingi milioni 320 kijiji cha Kasenda Chato.
 Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu akifurahi na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel baada ya makabidhiano ya Soko la Samaki la Kimataifa lililopo kijiji cha Kasenda Kata ya Mganza Wilaya ya Chato.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Mhandisi Robert Gabriel(kushoto) na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Yoshida Masaharu  wakisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kijiji cha Kasenda kwa ajili ya Makabidhiano ya Mradi wa Soko la Samaki la Kimataifa na kusaini mkataba wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa Kilometa 1 ya kutoka Mganza kwenda Kasenda.
 Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mheshimiwa Yoshida Masaharu na Viongozi wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato baada ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Soko la Samaki la Kimataifa la Kasenda Wilayani Chato.Watatu kutoka kushoto kwa balozi ni Waziri wa Nishati (Mb) Mheshimiwa Medard Kalemani na Shaban Ntarambe Mkuu wa Wilaya ya Chato na Kulia kwa balozi aliyevaa miwani na suti ya kijivu ni Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel pamoja na Bw; Joel Hari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato.
 Mradi wa ujenzi wa Soko la kimataifa la Samaki la Kijiji cha Kasenda Wilayani Chato uliojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Waziri wa Nishati (Mb) Medard Kalemani (wa kwanza kulia) akijadili jambo pamoja na Mheshimiwa Balozi Yoshida Masaharu, Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita na Bathromeo manunga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato

No comments: