Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiongea na baadhi ya viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Isoliwaya wakatika wa kukabidhi msaada huo kwa ajili ya kujengea vyoo ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho Leah Moto na Nancy Nyalusi walikuwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41 ya chama cha mapinduzi
Hili ni moja ya jengo lashule ya msingi Ilula iliyopo katika tarafa ya mazombe wilayani kilolo mkoani Iringa
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiwa katika kusherekea miaka 41 ya kuzaliwa chama chao kwa kufanya shughuli za kijamiii
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Shule
hizo zilizotenganishwa baada idadi kubwa ya wanafunzi, walimu 49 wanalazimika
kutumia choo Chenye matundu mawili hali inayohatarisha usalama wa afya zao.
Akizungumza
mbele ya Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith
Laizer, mwalimu Msaidizi wa shule ya Msingi Isoliwaya, Huruma Mbena alisema
hali hiyo inahatarisha afya za walimu kutokana na changamoto hiyo.
Mbena
alisema kuwa baada ya shule hizo kutenganishwa vyoo vya walimu vilibaki kwa
shule ya Ilula hivyo kutokana na idadi kubwa ya walimu wanalazimika kutumia
vyoo hivyo licha ya kutotosheleza kutokana na idadi kubwa ya walimu.
Aidha
alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya nyumba za walimu ambao
hadi sasa walimu 21 wanaishi katika nyumba za kupanga hali inayowaletea ugumu
wa maisha zaidi.
Alisema
kuwa changamoto nyingine wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa ofisi za walimu na
ofisi ya mwalimu mkuu na kulazimika kutumia moja ya darasa kama ofisi na
kupunguza idadi ya madarasa.
Akijibia hoja
zilizopo kwenye risala Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo
Judith Laizer alisema kuwa umoja huo umewaleta mifuko ya saruji kumi na tano
(15) na bati saba kwa ajili ya kusaidia kujenga vyoo vya walimu ili kupunguza
adhabu wanayoipata.
“Kweli ukikosa
huduma ya choo bora walimu hawezi kuwa huru kufundisha wanafunzi maana anaenda
chooni huku akijua kuwa wanafunzi wake wanamtazama kwa mtazamo tofauti na
ukizingatia maisha ambayo wanaishi majumbani kwao” alisema Laizer
Laizer
alisema kuwa changamoto nyingine kama ukosefu wa nyumba za walimu,upungufu wa
vyumba nane vya madarasa na ukosefu wa ofisi ya walimu atazifikisha kwa
viongozi wa wilaya na kwa mbunge wa jimbo hilo Vennace Mwamoto.
“Hizi changamoto
zenu zinatatulika kwa kuzingatia kuwa vingozi wa wilaya hii ni wachapakazi na
waadilifu kuwatumikia wananchi nauhakika kuwa watakuja hapa na kuzitafutia
ufumbuzi hizi changamoto kwa kuwa nitazifikisha kama nilivyozichukua hapa”
akisema Laizer
Lakini Laizer
aliwataka viongozi wa bodi ya shule hilyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu
na wazazi wa shule hiyo kwa kuhakikisha wanaanza ujenzi wa nyumba za walimu pamoja
na kujenga vyumba vya madarasa na mwishoni mbunge na halmshauri watamalizia
sehemu iliyobaki.
“Naombeni
nyie viongozi kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi hao bila kuwashirikisha
walimu kwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
kama alivyoagiza kuwa elimu bure bila malipo” alisema Laizer
Laizer aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kubwa ya
kufaulisha kwa wastani unaolidhisha na kuwaomba kuongeza bidii kufundisha huku
wakibuni mbinu mpya za ufundishaji.
No comments:
Post a Comment