Advertisements

Saturday, February 24, 2018

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF akutana na Makamu wa Rais mkoani Simiyu


Mkurugenzi Mkazi wa shirika la AMREF Dr.Florence Temu akitoa salamu zake kwa Makamu wa Rais, kabla ya kukutana kwenye kikao cha ndani kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan leo ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu ambapo pamoja na kukagua shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo, pia amekutana na wadau wa maendeleo wanaotekeleza miradi ya maendeleo mkoani humo.

Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na shirika la AMREF Health Africa ambapo makamu wa Rais Mhe.Suluhu amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo Dr.Florence Temu. Ziara ya Makamu wa Rais iliyoanza jumapili Februari 18,2018 mkoani Simiyu inatarajia kufikia tamati kesho alhamisi.

Shirika la AMREF linatekeleza mradi wa Uzazi Uzima unaofadhiliwa na shirika la Global Affairs Canada (GAC) pamoja na washirika wengine ambao ni Marie Stopes Tanzania na Deloitte ambapo mradi huo unatekelezwa katika halmashauri za Bariadi Vijijini, Bariadi Mjini, Busega, Itilima, Meatu pamoja na Maswa ukilenga kuboresha huduma za afya ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
\

Mkurugenzi Mkazi wa shirika la AMREF Dr.Florence Temu akitoa salamu zake kwa Makamu wa Rais, kabla ya kukutana kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Bariadi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu. Na BMG

No comments: