ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 15, 2018

Polisi kumchunguza Freeman Mbowe

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Murilo Jumanne Murilo amefunguka na kusema kuwa jeshi hilo sasa linachunguza kauli alizotoa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kuhusu kifo cha Kiongozi wa CHADEMA kata ya Hananasif, ambaye mwili wake uliokotwa ukiwa na majeraha.

Kamanda Murilo amesema haya jana  Februari 14, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ikiwepo suala la uchaguzi na kusema kuwa wao kama jeshi la polisi wanachunguza taarifa alizotoa Mbowe kuhusu sakata la kifo cha kiongozi huyo wa CHADEMA.

"Moja ya kazi kubwa ya jeshi la polisi ni kuchunguza jambo hiyo ni kauli yeye ametoa na kauli yake tunaichunguza pia anasema hivyo kwa kuzingatia misingi ipi ambayo inamsukuma yeye kusema hayo anayoyasema...

"Hatuwezi kuacha mtu akajisemea vitu kwa kusukumwa na hisia zake ndiyo maana sisi jambo linapotokea jambo la kwanza kabisa kufanya ni kuchunguza.... hatusukumwi na hisia za mtu kwa sababu tunajua yeye hajasomea kazi ya polisi na hayo anayotamka tunayachukua kama taarifa zingine za kawaida ambazo mwananchi yoyote anaweza kutupa" alisema Murilo


Aidha Murilo aendelea kudai kuwa wamekuwa wakimsikia sana Mbowe akitoa kauli mbalimbali

"Mhe. Mbowe tunamfahamu sana amekuwa akitoa matamko mengi mbalimbali hivyo jukumu letu ni kuchunguza itakavyo lazimika sisi tutamuomba atueleze anamaanisha nini kutamka hivyo itakavyolazimika lakini hatuwezi kusukumwa na kauli yake, tukatoka kwenye msingi wa upelelezi na kuburuzwa na hisia zake halafu baadaye tukosee ili haki isitendeke. Nachoweza kusema wahalifu wote tukichunguza na kuthibitisha huwa wanakamatwa"

No comments: