ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 1, 2018

Ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini (Jamhuri ya Korea)


Mheshimiwa Matilda Masuka Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea akiwakaribisha na kuwashukuru wageni waalikwa waliohudhuria kwa wingi kwenye ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi tarehe 31 Januari 2018. Awali Tanzania ilikuwa inawakilishwa nchini humo kutokea Japan. Mheshimiwa Balozi Matilda Masuka aliteuliwa Desemba 3, 2016 na baadaye kuapishwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake Mji Mkuu wa Seoul, Jamhuri ya Korea.


Mheshimiwa Lim Sung-nam, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea akizungumza kwa niaba ya Serikali yake wakati wa ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Kwenye salamu zake za ufunguzi, Mheshimiwa Sung-nam amesifu jitihada za Serikali ya Tanzania kukuza uchumi na kusifu ushawishi na karisma ya Balozi Masuka ambayo imewezesha kuvutia Mabalozi na wanadiplomasia wengi Jijini Seoul kushuhudia ufunguzi wa ofisi za Ubalozi.


Mheshimiwa Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu akihutubia wageni waliofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania. Mheshimiwa Ki-moon, ambaye alitambulishwa kama rafiki mkuu wa Tanzania nchini humo, alipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanikiwa kusimika bendera ya Tanzania nchini mwake baada ya miaka 25 ya uhusiano mzuri wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi.


Picha ya pamoja baada ya Waziri Mahiga na Mheshimiwa Sung-nam kukata utepe na kuzindua rasmi majengo hayo. Kutoka kushoto ni Bw. Park Young min, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afrika; Mhe. Silvester Bile, Kiongozi wa Mabalozi wa Afrika na Balozi wa Ivory Coast; Mhe. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu; Mhe. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania; Mhe. Lim Sung-nam, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Korea Kusini; Mhe. Matilda Masuka, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini; na Mhe. Salim Alharthy, Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa Falme ya Oman nchini Korea ya Kusini.


Picha ya pamoja na Mabalozi wanawake wanaoziwakilisha nchi mbalimbali kwenye Jamhuri ya Korea


Picha ya Mabalozi kutoka nchi za kiafrika walioko nchini Korea Kusini.

No comments: