ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 10, 2018

Ukuta wa migodi ya tanzanite kukamilika Aprili

Ukuta wa Mererani wenye urefu wa Kilomita 25 unaojengwa na SUMAJKT
UJENZI wa ukuta kuzunguka Mgodi wa Tanzanite Merereni, mkoani Manyara wenye mzunguko wa kilomita 24.5 unaratajiwa kukamilika mwishoni mwa Aprili, mwaka huu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliliambia Bunge na Watanzania wote mjini Dodoma jana wakati akiahirisha Mkutano wa 10 kwamba, ujenzi wa ukuta huo UJENZI wa ukuta kuzunguka Mgodi wa Tanzanite Merereni, mkoani Manyara wenye mzunguko wa kilomita 24.5 unaratajiwa kukamilika mwishoni mwa Aprili, mwaka huu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliliambia Bunge na Watanzania wote mjini Dodoma jana wakati akiahirisha Mkutano wa 10 kwamba, ujenzi wa ukuta huo upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Alisema Septemba 20, mwaka jana, Rais John Magufuli alitoa agizo la ujenzi wa ukuta katika eneo linalozunguka mgodi huo ili kuimarisha ulinzi na kudhibiti utoroshaji wa madini hayo, jambo ambalo limetekelezwa kwa kiwango hicho.

Kuhusu mwenendo wa uwekezaji kupitia wachimbaji wadogo, Waziri Mkuu alisema, serikali inaendelea na mkakati wake wa kuimarisha uwekezaji katika rasilimali za madini kupitia wachimbaji wadogo.

Aidha, tangu mwaka 2000 hadi kufi kia Desemba mwaka jana, kuna jumla ya leseni hai za uchimbaji mdogo 33,920 katika nchi nzima, kati ya hizo, leseni 6,976 zilitolewa kuanzia mwaka 2016/17 hadi hivi sasa.

Alisema serikali imetenga maeneo 46 yenye ukubwa wa jumla ya hekta 281,534 kwa ajili ya wachimbaji mbalimbali. “Mpango wa serikali ni kuwekeza katika utafutaji madini katika maeneo yaliyotengewa ili taarifa ziwasaidie wachimbaji wadogo katika utekelezaji wao,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa mwito kwa wachimbaji wadogo kuunga mkono juhudi za serikali kuwasaidia wachimbaji hao, kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchimbaji madini kwa ajili ya usalama, afya na utunzaji wa mazingira, lakini pia wanatakiwa kutekeleza wajibu wao wa kulipa tozo stahiki.

Kuhusu utatuzi wa migogoro katika maeneo ya machimbo, Waziri Mkuu alisema serikali inaendelea na juhudi za kutatua migogo katika meneo mbalimbali ya machimbo ukiwemo mgogoro wa Nyamongo, mkoani Mara dhidi ya mwekezaji Kampuni ya North Mara.

Kuhusu Tume ya Madini, Waziri Mkuu alisema kuwa uundaji wa Tume ya Madini unaendelea, aidha Katibu Mtendaji wa Tume hiyo ameshateuliwa na kikao cha kwanza cha makamishna wa Tume kilifanyika Januari 6, mwaka huu.

Alisema katika kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipitia mapendekezo ya uteuzi wa wafanyakazi katika nafasi mbalimbali ndani ya Tume hiyo. “Hata hivyo, kazi za msingi za Tume kama utoaji wa vibali vya kusafi risha madini nje ya nchi vinatolewa kwa usimamizi wa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo,” alisema.

HABARI LEO

No comments: