Na Tiganya Vincent-rs Tabora
Vitambulisho wa uraia vitasaidia kuwa na utambuzi wa wananchi utakao ondoa ile tabia ya baadhi ya watu kutilia mashaka wakati wa shughuli mbalimbali ikiwemo kipindi kushiriki katika zoezi la uchaguzi wote wote.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.Mwigulu Nchemba wakati uzinduzi wa zoezi la usajili wananchi kwa ajili ya vitambulisho vya kitaifa mkoani humo.
Alisema kuwa mara nyingi mtu anapogombea nafasi yoyote hapa nchini au kunapokuwepo na migogoro ya kugombania mashamba ndio suala la kusema kuwa huyo sio raia linapojitokeza.
Dkt. Nchemba alisema wananchi wenye sifa kuchangamkia zoezi la usajili na upataji wa vitambulisho vya uraia ili kuepuka matatizo kama vile migogoro ikiwemo ya mapingamizi wakati chaguzi mbalimbali na kuiweza Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wake
Alisema kuwa hata uchumi wa kisasa unaanza na kutambua kwa Serikali kutambua watu iliyonao na ndipo ipange mipango ya maendeleo kwa ajili yao.Waziri huyo aliongeza kuwa hata kwenye vyombo vya fedha kama vile Benki zimekuwa zikiweka riba kubwa katika mikopo kwa sababu ya baadhi wananchi kukosa utambulizi
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Andrew Massawe alisema jitihada hizi zote zimelenga kusaidia Serikali na wananchi kutambulika na hatimaye Mashirika, Taasisi na Makampuni nchini kutumia mfumo huu kutoa huduma zenye ubora na tija kwa Taifa.
Alisema mfumo huu una faida nyingi kwa Taifa na mwananchi mmoja mmoja kama vile kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi, wananchi kutambulika kwa haraka pindi wanapofika kupata huduma za afya na Elimu.
Massawe alisema kuwa faida nyingine ni kurahisisha utambuzi wa makundi yenye mahitaji maalumu ikiwemo utambuzi wa kaya masikini unaofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na upatikanaji wa huduma za kifedha na Simu kirahisi.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi aliwaagiza viongozi wa ngazi zote mkoani humo kuhakikisha kuwa anayesajiliwa na kupata kitambulisho cha uraia ni yule mwenye sifa na sio mgeni.
Alisema Serikali ya Mkoa wa Tabora haitasita kumchukulua mtu yoyote atayeshiriki katika udanganyifu utaosababu watu wasio raia kupata vitambulisho vya uraia.
Queen alisema kuwa kila mmoja ni vema akasimama katika nafasi yake kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu ili kuleta ufanisi.
Alitoa wito kwa jamii kusaidia kuwafichua watu wasio raia wanaotaka kujipenya ili wapate vitambulisho vya uraia
No comments:
Post a Comment