ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 7, 2018

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WIZARA YA NISHATI MH.SUBIRA MGALU MKOANI KILIMANJARO

Tarehe 24 - 26/01/2018 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini (REA II & REA III) kwenye jumla ya vijiji 18 katika wilaya za ROMBO, MWANGA NA SAME Mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongea na wananchi, pia kutambulisha wakandarasi wa miradi ambapo aliwaagiza wakandarasi waepuke kurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.

Pia Katika ziara hiyo Mh. Naibu waziri alitembelea bwawa la kuzalisha umeme la NYUMBA YA MUNGU kujionea shughuli za uzalishaji.

Mh Naibu waziri amemaliza ziara yake 26/01/2018 saa 12:00 jioni na kuelekea mkoani TANGA.

RCRO KILIMANJARO.
Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mkisha kuhusu kifaa kijulikanacho kama UMETA (REDY BODY) kifaa hicho hutumika kama mbadala wa kusuka mifumo ya waya (wiring) ndani ya nyumba. Aliyeshika kifaa hicho ni Afisa uhusiano TANESCO KILIMANJARO Bw. Samuel Mandari.
Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasikiliza wanakijiji na kueleza uhitaji wa huduma ya umeme.
Wanakijiji wakimsikiliza Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) akieleza uhitaji wa huduma ya umeme.
Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule, Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, wakiwa na viongozi wa TANESCO MKOA wa Kilimanjaro walipo tembelea Kijiji cha Vunta wilayani Same.

No comments: