Baada ya tetesi kuvuma zilizo jaa ukweli kuhusiana na Mama wanamitindo
maarufu hapa Tanzania, Asya Idarous Khamsin kustaafu kuandaa jukwaa la ‘Lady In
Red.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa King Solomon Asya amesema kuwa Jukwaa la
Lady in Red mpaka sasa limedumu kwa muda wa miaka 15 likiwa chini yake. Pia alifafanua dhamira ya jukwaa la Lady in Red ambapo
alisema jukwaa hilo lilianzishwa kwa lengo la kukuza vipaji vipya kwenye Tasnia
ya Mitindo hapa Tanzania, ndio maana jukwaa asilimia kubwa huwa linapandisha
upcoming Designers maana ndio jukwaa lao la kujidaia.
Aidha aliongeza kuwa kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red
haimaanishi kwamba ataachana na mambo ya ubunifu, “siwezi kuacha maana ndio
kazi inayo niweka mjini” alisisitiza Asya.
“Kilicho kikubwa nimeamua kutoa fursa kwa wanamitindo ambao wamekulia
kwenye jukwaa hilo”.
Kumbuka Lady in Red 2018 itafanyika 9/Feb/2018 katika ukumbi
wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es salaam. Siku hiyo ndipo Asya atakapojivua kuandaa na kukabidhi Designers wengine jukwaa hilo.
No comments:
Post a Comment