ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 23, 2018

KATIBU MTENDAJI BODI YA FILAMU AFANYA ZIARA YA MKOANI SHINYANGA

 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (kulia) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msevela (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo. Bi Joyce Fissoo yupo mkoani Shinyanga kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke iliyoandaliwa na kikundi cha sanaa cha Bongo Movie Shinyanga.
 Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga, Mariam Ally akizungumza na umoja wa Chama cha Wasanii wa mkoa wa Shinyanga wakati wa mafunzo ya uandaaji wa filamu yaliyofanyika leo. Mafunzo haya ni sehemu ya utangulizi kabla ya uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke iliyoandaliwa na kikundi cha sanaa cha Bongo Movie Shinyanga utakaofanyika baadae hii leo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kuandaa filamu yaliyofanyika mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Shinyanga, Saidu Miraji na Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga, Mariam Ally. Bi Joyce Fissoo yupo mkoani humo kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke iliyoandaliwa na kikundi cha sanaa cha Bongo Movie Shinyanga utakaofanyika baadae hii leo.

No comments: