Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho
kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa
Maithripala SIRISENA.
Hii
ni hatua muhimu katika kuendeleza, kuimarisha na kukuza uhusiano wa kirafiki na
ushirikiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Sri Lanka ambao ulianza mnamo
miaka ya tisini. Wakati huo, Sri Lanka ilikuwa inawakilishwa nchini Tanzania
kupitia Ubalozi wake wa mjini Kampala, Uganda ambao baadaye ulifungwa na
Tanzania ikiwakilishwa nchini Sri Lanka kupitia Ubalozi wake wa New Delhi. Kwa
sasa Sri Lanka inakusudia kumteua Balozi wake mjini Nairobi ambaye pia
ataiwakilisha nchi hiyo nchini Tanzania.
Katika
hafla hiyo, Balozi Luvanda aliambatana na Mwambata Jeshi wa Tanzania nchini
India, Col. Amri Salim MWAMI. Aidha,
Balozi Luvanda alifanya mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Sri Lanka pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika, ambapo ameahidi kushirikiana kwa
karibu na watendaji hao katika kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi
mbili na ambao utazinufaisha zaidi, hususan katika kuhakikisha uhaulishaji wa
uzoefu, teknolojia na utaalam wa Sri Lanka kwa Tanzania kwenye sekta ya viwanda
vya nguo, madini na vito mbali mbali na kilimo.
Sri
Lanka ni nchi yenye uchumi unaoendelea ingawa imepitia kipindi kigumu cha vita
vya wenyewe kwa wenyewe kwa takriban miaka 25, vita ambavyo vilimalizika mwaka
2009.
|
No comments:
Post a Comment