Advertisements

Saturday, April 14, 2018

Hukumu ya Nabii Tito Kutolewa April 20

Hukumu ya kesi ya Tito Machibya (maarufu Nabii Tito), ambayo ilikuwa itolewe uamuzi jana, iliahirishwa hadi Aprili 20, mwaka huu kutokana na hakimu anayehusika na kesi hiyo kuwa na dharura.

Akitoa maelezo mahakamani hapo, Mwanasheria wa Serikali Judith Mwakyusa, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Godfrey Pius, alisema kesi hiyo ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo.

Mwakyusa alisema kesi hiyo ilikuwa itolewe uamuzi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha, lakini amepata dharura.

“Mheshimiwa Hakimu shauri hili limeletwa kwako kwa ajili ya kuahirishwa kutokana na Karayemaha kuwa na dharura,” alisema.Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Pius, aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20, mwaka huu itakapoletwa tena kwa ajili ya uamuzi.

Pius alisema mtuhumiwa atarudishwa rumande hadi tarehe hiyo.

Aprili 5, mwaka huu Hakimu Karayemaha alisema wamepokea taarifa ya kitabibu kutoka taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga inayomhusu Mchibya na uamuzi ungetolewa jana.

Nabii Tito alidai ana matatizo ya akili yaliyosababisha kutaka kujiua na kuiomba mahakama kuamuru akachukuliwe vipimo ili kupata uhakika wa afya yake ya akili.

Katika kesi hiyo, anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo, Januari 25, mwaka huu katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.

No comments: