ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 26, 2018

Ufunguzi rasmi wa maonesho ya kipekee ya bidhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya

Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwangi Kiunjuri akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa wiki ya Tanzania nchini Kenya ambayo imeambatana na maonesho ya huduma, vivutio vya utalii na bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 28 Aprili 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (KICC) Jijini Nairobi, Kenya. 
Mhe. Waziri Kiunjuri akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Wiki ya Tanzania nchini Kenya ambayo itaenda sambamba na Maonesho ya bidhaa za viwanda, Kongamano la biashara na Maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Kenya tarehe 25 Aprili 2018.

Mhe. Wanjuri katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa kilimo cha kisasa ili kupata mazao yatakayokidhi vigezo vya ubora na kuingia katika ushindani wa biashara kimataifa utakaopelekea maendeleo ya uchumi hususan uchumi wa viwanda. 
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Wiki ya Tanzania nchini Kenya ambapo alieleza kuwa tukio hili ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya marais wa Tanzania na Kenya walipokutana katika Mkutano wa 19 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi rasmi wa wiki ya Tanzania nchini Kenya.
Katika ufunguzi huo Mhe. Chana alieleza umuhimu wa maonesho hayo ni pamoja na kuzitangaza huduma na bidhaa za viwanda vya Tanzania ili ziweze kupenyeza katika soko la Kenya. Maonesho hayo yametoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania kukutana na kufanya mazungumzo ya biashara na wafanyabishara kutoka katika kampuni za Kenya. 
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Katibu wa kamati ya maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega na mjumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Francis Mossongo wakifuatilia hafla ya ufunguzi. 
Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa hafla hiyo. 
Sehemu nyingine ya wafanyabiashara wakifuatilia hafla ya ufunguzi huo. 
Sehemu ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini Kenya wakifuatilia hafla ya ufunguzi. 
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini Kenya wakifuatilia hafla ya ufunguzi. 
Wajumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia hafla hiyo. 
=======================================================================
Wakati huo huo Mhe. Waziri Kiunjuri alitumia fursa hiyo kukabidhi vyeti kwa washiriki pamoja na kutembelea mabanda ya maonesho.
Mhe. Waziri Kiunjuri akikabidhi cheti cha ushiriki kwa mwakilishi wa kampuni ya Lake Group, Bw. Peter Sifa 
Mhe. Waziri wa Kiunjuri akimkabidhi cheti cha ushiriki mwakilishi kutoka Kampuni ya vinywaji (Tanzania Distillers Ltd)
Mhe. Waziri Kiunjuri akikabidhi cheti cha ushiri kwa mmoja wa wafanyabiashara kutoka Zanzibar, Bw. Nassoro Omar wa Kampuni ya ZANOP. 
Mhe. Kiunjuri akimkabidhi cheti mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maonesho na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka. 
Mhe. Waziri Kiunjuri akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na mwenyekiti mwenza wa kamati ya maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya, Bw. Godfrey Simbeye kwa kufanikisha zoezi la uratibu wa wiki hiyo. 
Mhe. Waziri Kiunjuri akipokea maelezo kwa mmoja wa washiriki wa maonesho ya bidhaa kutoka Tanzania, Bw. Amir Esmail kutoka kampuni ya kahawa ya AMIMZA.

No comments: