ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 1, 2018

'Waganga wa jadi saidieni wajawazito waende kliniki'

Tokeo la picha la WAGANGA WA JADI
WAGANGA wa jadi nchini wametakiwa kutimiza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutakiwa kuwaelekeza wajawazito wanaowapokea kwa ajili ya kuwahudumia wahudhurie kliniki jambo litakalowasaidia kubaini endapo kuna viashiria vyenye hatari.

Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga nchini (TNMC), Lena Mfalila alisema hayo jijini Dar es Salaam katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu Duniani (UNFPA) kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kufahamu umuhimu wa wanataaluma hao.

Kuhusu wakunga wa jadi alisema baraza hilo limekuwa likiwatambua kuwa wanahusika kufuatilia wajawazito katika maeneo mbalimbali, lakini ni kundi ambalo halina maarifa wala mawazo mbada pale mjamzito anapokuwa katika wakati mgumu.

“Tuliwaingiza waganga wa jadi katika Baraza letu kwa mujibu wa sheria kwa kuwa wapo wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyoko mbali na hospitali lakini, waganga hao wakitakiwa kutoa ujumbe maalum wa kuwaelekeza wajawazito kuona umuhimu wa kuhudhuria hospitali kwa ajili ya huduma nyingine,” alisema Lena.

Kuhusu hali za wakunga na wauguzi nchini, alisema Baraza hilo limehuisha mtaala na kuweka viwango na vigezo vya juu vya kusomea taaluma hiyo, lengo likiwa ni kupandisha hadhi ya taaluma hiyo ambayo kila mara imekuwa ikisemwa midomoni mwa wananchikuwa ni moja yakundi lisilo tii na maadili ya kazi.

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Huduma, kutoka TNMC Happy Masenga alisema huduma ya uuguzi na ukunga ni taaluma ya pekee kwani inahusika kwa namna ya pekee katika kudhihirisha uumbaji katika kulinda usalama wa afya ya watu, jamii na Taifa nzima.

Alisema ni vema kutambua kuwa, katika vituo vya kutolea huduma wapo wataalamu wengine wa afya wanaoshiriki kwa njia nyingine katika kufanikisha huduma za afya zinazotolewa kwa wateja wa huduma za afya ambapo muuguzi na mkunga ndiye anayebeba jukumu kubwa kwa kuwa ndiyo wanakuwa na wagonjwa kwa saa 24 na siku saba za wiki.

HABARI LEO

No comments: