Advertisements

Thursday, May 3, 2018

KALEMANI, MGALU WAONGOZA KIKAO CHA MAJADILIANO YA MAENDELEO MRADI WA LNG

Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu wameongoza kikao kilichojadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG).
Kikao hicho kilifanyika Aprili 30 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kushirikisha Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na wataalamu kutoka wizarani.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Subira Mgalu.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu (kushoto), wakiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi, wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wajumbe kutoka TPD, EWURA na PURA.

 
 Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na  wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wakiwa katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na  wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, muda mfupi kabla ya kuanza kikao baina yao kujadili maendeleo ya Mradi huo.

No comments: